MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka watumishi wa afya Mkoa wa Shinyanga kufanya kwa weledi, maarifa na kwa kuzingatia miiko ya taaluma zao na kuwa na hofu ya Mungu.
RC Mndeme ameyasema haya leo tarehe 25 Januari, 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Manispaa Kahama alipokuwa akitana na watumishi kutoka Halmashauri za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama kama sehemu ya kuwakumbusha wajibu wao na kuagiza wale wanaobainika kwenda kinyume na misingi ya kazi zao wawajibishwe kisheria nasio vinginevyo.
Pamoja na angalizo hilo, Mhe. Mndeme pia amesema hivi karibuni kuna watumishi wa kutoka Idara ya Afya katika Hospitali ya Manispaa Kahama, watumishi walisimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu na uzembe uliyosababisha kifo cha mama mjamzito na mtoto wake usiku wa tarehe 29 Januari, 2023.
RC Mndeme amesema , serikali imekuwa ikitengeneza mazingira mazuri ya kutolea huduma lakini wachache wasiokuwa na maadili ya kazi wanaichafua sekta hii kwa kufanya vitu vya hovyo.
Katika hatua nyingine, RC Mndeme amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga kuwaondoa kwenye nafasi zao Mganga Mkuu wa Manispaa na Mganga Mfawidhi wa Manispaa ya Kahama kwa kushindwa kusimamia vema majumu yao yaliyopelekea uzembe kwa watumishi wa afya Kahama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa