Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta za Umma
Start Date: 2016-03-09
End Date: 2020-01-09
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma unatekelezwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI kwa kushirikiana na Kampuni Binafsi ya Kimarekani inayojulikana kwa jina la Abt Associates Inc ambayo makao yake makuu kwa hapa Tanzania yapo Dar es Salaaam. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa ufadhili wa Dola za Kimarekani Milioni 62. Mradi huu utatekelezwa katika Halmashauri 96 zilizopo katika Mikoa 13 ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Kigoma, Dodoma, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Lindi na Mtwara.
Lengo la mradi huu ni kuisaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha Mifumo katika Sekta za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kutoa mwongozo juu ya uimarishaji wa Mpango Mkakati, Uboreshaji na Utekelezaji wa huduma za kijamii kama vile Afya, Elimu, Kilimo n.k.
Mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wafuatao;-
Benjamin Mkapa Foundation (BMF)
Chuo cha Serikali za Serikali za Mitaa (LGTI)- Hombolo