Katika kuadhimisha Siku ya Usafishaji Duniani Septemba 20, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita ameongoza mamia ya wananchi kushiriki zoezi la usafi katika Soko la Kambarage, Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza na wananchi, Mhe. Mhita amesisitiza umuhimu wa kuzingatia usafi kama sehemu ya maisha ya kila siku na si tukio la mara moja.
Ameeleza kuwa soko hilo ni miongoni mwa maeneo yatakayofanyiwa maboresho kupitia mradi wa TACTIC, hivyo kuhitaji maandalizi bora ya mazingira.“Tuache kusubiri maagizo, tufanye usafi kwa kujitambua, kwa afya zetu, kwa heshima ya mji wetu,” amesema RC Mhita.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni amepongeza mwitikio wa wananchi na kutoa wito kwa jamii kuendeleza utamaduni huo kila siku.
Katika uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara uliofanyika Septemba 10, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita ameitaka TRA kutumia njia za maelewano na elimu badala ya kufunga biashara kwa changamoto zinazoweza kutatuliwa.
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yalikuwa jukwaa la kipekee kwa Mkoa wa Shinyanga kuonesha fursa za kiuchumi, mafanikio ya miradi ya kimkakati, ubunifu wa wananchi na ushiriki wa taasisi mbalimbali.
Kupitia Makala hii, tunakuletea kumbukumbu ya maandalizi na msisimko kuelekea Sabasaba, tukionesha dhamira ya Mkoa wa Shinyanga katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi wa viwanda na biashara.
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa