Katika uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara uliofanyika Septemba 10, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita ameitaka TRA kutumia njia za maelewano na elimu badala ya kufunga biashara kwa changamoto zinazoweza kutatuliwa.
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yalikuwa jukwaa la kipekee kwa Mkoa wa Shinyanga kuonesha fursa za kiuchumi, mafanikio ya miradi ya kimkakati, ubunifu wa wananchi na ushiriki wa taasisi mbalimbali.
Kupitia Makala hii, tunakuletea kumbukumbu ya maandalizi na msisimko kuelekea Sabasaba, tukionesha dhamira ya Mkoa wa Shinyanga katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi wa viwanda na biashara.
Karibu utazame Makala maalum ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 katika Mkoa wa Shinyanga! Mwenge wa Uhuru umepita kwenye Halmashauri zote za Mkoa huu, ukikagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Kupitia Makala hii, utaona namna wananchi, viongozi na taasisi mbalimbali walivyoshiriki kwa pamoja katika kuenzi tunu ya Uhuru, Uwajibikaji na Maendeleo kwa wote.Makala hii inaonesha mshikamano, uwazi na jitihada za Serikali ya Mkoa wa Shinyanga chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mboni Mhita, katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya wananchi kwa weledi na uaminifu.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa